Maranatha Media Kenya

Vitabu

Agape

Ndani ya kila mmoja wetu ni hamu ya Amani, utulivu na dhibitisho la kupendwa. Ni jinsi gani jamii ya mwanadamu inaweza ukaribia uhalisia huu? Na maendeleo haya yote katika teknolojia ulimwengu wetu yanaingia ndani zaidi katika ubinafsi na ukatili.

Maisha ya Kristo ambaye alitembea duniani miaka 2000 iliyopita yanatupa mfano wa upendo wa kujikana nafsi ambao umeleta amani kwa mamilioni yasiyohesabika. Kwa watu wengi upendo huu mzuri huangamizwa na hata kuharibiwa na hadithi nyingi ambazo zimenakiliwa katika kurasa za Bibilia zikielezea uhusiano wa Mungu na watu katika historia yote ya mwanadamu.

Baba yetu Mpenda Rehema

Baba yetu Mpenda Rehema

Matendo ya Mungu Wetu Mpole

Matendo ya Mungu wetu mpole yanawasilisha ushahidi wa kutosha kuaminika kutoka kwenye Bibilia wa kumuondolea Mungu mashtaka kuwa yeye ni asiyejali, mwenye kuhukumu, mwenye kudhibiti, asiyehaki, mwenye hamaki, au katili. Kitabu kinadhihirisha kwamba Bibilia nzima, ikieleweka kwa usahihi, iko katika uiano na kifungu elezi: “Mungu ni Upendo” (1 Yohana 4:8)

Mfariji

Adamu alikabiliwa na chaguzi wakati mke wake alipomletea tunda lililokataliwa kwake. Alipochagua kukubali jaribio na kumfuata mkewe alimkataa Muumbaji wake. Je, nani sasa angekuwa chemichemi ya utulivu? Hawa alitolewa kwa Adamu ili awe msaidizi wake. Je, angeweza kumsaidia kukabiliana na mabadiliko yaliyotokana na kumuasi Mungu? Je, kuanguka dhambini kwa mwanadamu kulibadili vipi muungano huu? Je hili lilibadili vipi kipaji cha uzazi( tendo la ngono) kuhusiana na lile agano la zaeni mkajaze dunia?

Mpendwa Wangu

Nasikia hatua zake, mapigo yangu ya moyo yanaenda kwa kasi kwa matarajio. Naisikia sauti yake kama mlio wa maji mengi. Ni kama zeri tamu nafsini mwangu. Mpendwa wangu anaita; inaweza kuwa ni kwa ajili yangu anaita? Ni vipi tumaini la thamani kama hilo linaweza kuzwa kifuani mwangu? Dhana hii inaibuka kutoka wapi? Mbona nihesabiwe kwamba nastahili utambuzi wake—Mfalme huyu mkuu, Mwana Mpendwa wa Baba? kwa huwahi ya patakatifu, Wimbo ulio bora na Mwendo wa Safari (Pilgrim’s Progress) tunaelezea safari ya mtu mmoja kupitia kwa vizingiti, majaribu na changamoto, kutambua, kuuza vyote na kuwa na upendo na Yesu, Mwana wa Baba.

Msalaba Uliotahiniwa na Msalaba Ulioshuhudiwa

Mbona msalaba ulihitajika na nani aliuhitaji?

Mbona msalaba ulikuwa muhimu kwa ukombozi wetu?

Je, ghadhabu ya Mungu iliridhishwa na kifo cha Mwanawe?

Haki ya Mungu ni nini na ina tofauti na haki yetu?

Mbona Yesu alijilinganisha na Nyoka wa shaba juu ya mti?

Patakati pa Waisraeli panatwambia nini kuhusiana na Msalaba?

Silaha za kuchinja za Ezekieli tisa

Naye Bwana akasema kwake, nenda kati ya mji na ukaweke alama kwenye vipaji vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. (5) Na hao wengine aliwaambia nami nilisikia, piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; (6) Waueni kabisa, mzee na kijana na msichana, na watoto wachanga, na wanawake, lakini msikaribie mtu yeyote aliye na alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Ezek 9:4­6

Theos

Katika Kutafuta Mwana Mzaliwa wa Kwanza

Uasi wa Kora

Ni nani aliyewatuma Kora, Dathani na Abiramu wakiwa hai shimoni?

Ufunuo 18 Mwanga Katika Hukumu

Baba yetu alikuwa hapo katika giza yao ya utenda dhambi, lakini Kristo aliteseka kama mmoja wetu.

Uhusiano wa Baba na Mwana kupitia Sura Yao

“Na sasa Mungu anamwambia Mwanawe,” Tufanye mtu kwa mfano wetu. ‘Kama Adamu alitoka kutoka kwa mkono wa muumba wake, alikuwa na urefu mrefu, na wa ulinganifu mzuri ... Hawa hakuwa mrefu kabisa kama Adamu. Kichwa chake kilifikia juu kidogo ya mabega yake. Yeye pia alikuwa mzuri - kamili katika ulinganifu, na mrembo sana. Hawa wawili wasio na dhambi… ”1SP 24.2

Vita vya Utambulisho

Vita vya utambulisho ni safari ya kujitambua binafsi. Ni makaribisho ya kujifunza kuhusu thamani yako katika muktadha wa mahusiano.

Maisha yetu yameshambuliwa na kelele ya ujumbe wa mara kwa mara ambao hutuambia kwamba mafanikio huja tu kutokana na kujidhibitishia wenyewe na kuthibitishia ulimwengu kuwa tuna kila kinachohitajika, kuwa tuna mambo sawa. Ni mfumo ambao hutufunza kuhisi kuwa na thamani na umuhimu wakati ambao tumefaulu na kufanikiwa kwa kiwango fulani. Matokeo ya mfumo huu yako na ushahidi kuwa sio mazuri. Mamilioni wako katika dhiki na mamia yanamaliza maisha yao katika kukata tamaa.

Nakukaribisha ujifunze hali ya kweli ya vita tulivyo ndani yake – vita vya utambulisho wa kile kinachofafanua thamani yetu na karama. Vigingi viko juu kwa kuwa ni uzima na mauti. Kitabu hiki kina safari yangu na kanuni nilizojifunza njiani. Uhuru ni kitu ambacho hutegemea lakini kitabu hiki kinaelezea barabara yangu kwa uhuru.