Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Sep 09, 2022
Vya kupakuliwa 451

Lugha Zingine

български език Čeština English Français Deutsch 國語 Русский Српски Español

Katika kitabu hiki Adrian Ebens anawasilisha njia ya baraka, ambayo inatiririka kutoka kwa Mungu kama chanzo cha uhai wote na ambayo inaweza tu kuhifadhiwa ikiwa kanuni mahususi na muhimu inatimizwa: utii. Uhusiano wa upendo kati ya Mungu na Mwanawe, ambao unajidhihirisha hasa katika kujisalimisha kwa hiari kwa Mwana kwa Baba, ni kanuni ya kimungu ambayo bila hiyo baraka hii haiwezi kuanzishwa.

Je, ungependa kujua jukumu lako ni lipi katika mkondo wa baraka na ni sehemu gani unayofaa? Je, unataka familia yako ipate baraka za Mungu kwa kiwango kubwa? Je, unataka kuwa na furaha?

Kitabu hiki kinafungua kutazama mtazamo wa juu zaidi wa muundo huu wa kiungu wa "mkondo wa baraka". Kwa msingi wa historia ya Biblia, inaonyesha umuhimu wa miundo ya familia iliyoimarishwa kimungu pamoja na matokeo ya jitihada za daima za Shetani za kuharibu njia hii ya baraka ili kuzuia baraka za Mungu ulimwenguni kwa ujumla na pia kwenye familia.

Katika kitabu hiki utapata majibu mengi, yakiwemo yale ambayo huenda bado maswali yake hayajaulizwa, kwa kuwa kanuni takatifu ya baraka bado haijatambuliwa kwa uwazi unaohitajika. Kwa hiyo, wale walio na njaa ya kiroho na wanataka kuzijua njia za Mungu vizuri zaidi, wanapendekezewa kusoma kitabu hiki kisicho na kifani. "Aha" uzoefu unaopatikana wa maisha ya furaha ni matokeo yasiyoepukika ya kitabu hiki.