Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Aug 16, 2019
imeandikwa Aug 16, 2019
Vya kupakuliwa 1,998

Vita vya utambulisho ni safari ya kujitambua binafsi. Ni makaribisho ya kujifunza kuhusu thamani yako katika muktadha wa mahusiano.

Maisha yetu yameshambuliwa na kelele ya ujumbe wa mara kwa mara ambao hutuambia kwamba mafanikio huja tu kutokana na kujidhibitishia wenyewe na kuthibitishia ulimwengu kuwa tuna kila kinachohitajika, kuwa tuna mambo sawa. Ni mfumo ambao hutufunza kuhisi kuwa na thamani na umuhimu wakati ambao tumefaulu na kufanikiwa kwa kiwango fulani. Matokeo ya mfumo huu yako na ushahidi kuwa sio mazuri. Mamilioni wako katika dhiki na mamia yanamaliza maisha yao katika kukata tamaa.

Nakukaribisha ujifunze hali ya kweli ya vita tulivyo ndani yake – vita vya utambulisho wa kile kinachofafanua thamani yetu na karama. Vigingi viko juu kwa kuwa ni uzima na mauti. Kitabu hiki kina safari yangu na kanuni nilizojifunza njiani. Uhuru ni kitu ambacho hutegemea lakini kitabu hiki kinaelezea barabara yangu kwa uhuru.