Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Apr 29, 2021
Vya kupakuliwa 525

Mbona Yesu alimwambia Petro aweke kando upanga wake lakini anawaambia walawi kupitia kwa kambi na kuwaua wale ambao walikataa kutubu?

Kut 32:26-28 ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa Bwana, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia (27) Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. (28) Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.

Na unapata nini kwa maoni haya?

Wale ambao walijihusisha katika kazi hii ya kuchinja, ingawa chungu, sasa walikuwa watambue walikuwa wakitenda juu ya ndugu zao na adhabu kamili kutoka kwa Mungu; na kwa utekelezaji wa kazi hii chungu, kinyume na hisia zao wenyewe, Mungu atahifadhi mibaraka juu yao. 1SP 252

Tunaweza leta aje uiano kwa vitu hivi?

Ajabu ya msalaba huelezea maajabu mengine yote. Katika nuru ambayo hutiririka kutoka Kalvari sifa za Mungu ambazo zilikuwa zimetujaza na hofu na uoga zinaonekana kupendeza na kuvutia. Rehema, huruma, na upendo zinaonekana kuchanganyika na utukufu, haki na uwezo. Tunapotazama ukuu wa enzi yake, juu na kuinuka zaidi, tunaona tabia yake katika dhihirisho la neema yake, na kufahamu, kuliko awali, umuhimu wa jina hilo la kupendeza, « Baba Yetu."  GC 652.1

Tuuchunguzapo msalaba tunaona kwamba kweli huduma ya mauti ni tukufu na inawakaribisha wale ambao wanaamini ahadi za Mungu katika Haki yake.