Maranatha Media Kenya

Karibu  Maranatha  media- Kenya.

Tuna furaha umefika hapa. Katika hii tovuti tunawapa vifaa vyetu bora kuhusu tabia ya Mungu wetu wa huruma na wa upendo - na unavyo soma, utafahamu kwa nini tunauhakika kwamba Mungu kweli ni upendo. Kuna mengi ambayo watu hawafahamu  kuhusu tabia ya Mungu - hata wakristo thabiti! Shetani amefanya juu chini ( na kwa mara nyingi amefaulu ) kwa kuwafanya watu waamini kwamba Mungu ana tabia yake ( Shetani) mwenyewe ambazo ni za hasira, kulipiza kisasi na mauaji baadala ya tabia za Mungu  mwenyewe ambazo tumeambiwa katika Biblia : upendo, mwingi wa rehema tena mwenye fadhili.

" Je, tuseme nini kuhusu hadithi za Biblia katika Agano la kale kwamba Mungu anaua na kuamrisha mauaji?" Unaweza kuuliza. Nasi pia tumejiuliza swala hilo - kwa sababu Mungu kama huyo halingani na Yesu aliyefunuliwa katika Agano jipya - tena hii ni wazo la kutatanisha kwa kila mtu anayetaka kuelewa kwa nini Mungu ni upendo.

Kile utakacho gundua katika hii tovuti, ni kwa sababu ya utafiti wa miaka  16 kutaka kujua kuhusu Mungu na Yeye ni nani kwa  uhakika. Kila kitabu kina dhihirisha uchunguzi wa Biblia kwa makini na kwa undani zaidi kuhusu mada iliyosalia. Ni tumaini letu kwamba ni baraka kwako kama ilivyo kwetu. Kuna uhuru na furaha kufahamu kwa uhakika ya kwamba Mungu wetu kweli ni Mungu wa upendo, na tunapendwa kwa undani na Yeye.