Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jul 14, 2020
Vya kupakuliwa 1,200

Nasikia hatua zake, mapigo yangu ya moyo yanaenda kwa kasi kwa matarajio. Naisikia sauti yake kama mlio wa maji mengi. Ni kama zeri tamu nafsini mwangu. Mpendwa wangu anaita; inaweza kuwa ni kwa ajili yangu anaita? Ni vipi tumaini la thamani kama hilo linaweza kuzwa kifuani mwangu? Dhana hii inaibuka kutoka wapi? Mbona nihesabiwe kwamba nastahili utambuzi wake—Mfalme huyu mkuu, Mwana Mpendwa wa Baba? kwa huwahi ya patakatifu, Wimbo ulio bora na Mwendo wa Safari (Pilgrim’s Progress) tunaelezea safari ya mtu mmoja kupitia kwa vizingiti, majaribu na changamoto, kutambua, kuuza vyote na kuwa na upendo na Yesu, Mwana wa Baba.