Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Mac 20, 2020
imeandikwa Mac 20, 2020
Vya kupakuliwa 1,591

Adamu alikabiliwa na chaguzi wakati mke wake alipomletea tunda lililokataliwa kwake. Alipochagua kukubali jaribio na kumfuata mkewe alimkataa Muumbaji wake. Je, nani sasa angekuwa chemichemi ya utulivu? Hawa alitolewa kwa Adamu ili awe msaidizi wake. Je, angeweza kumsaidia kukabiliana na mabadiliko yaliyotokana na kumuasi Mungu? Je, kuanguka dhambini kwa mwanadamu kulibadili vipi muungano huu? Je hili lilibadili vipi kipaji cha uzazi( tendo la ngono) kuhusiana na lile agano la zaeni mkajaze dunia?

Kuongezeka kwa ponografia kupitia mitandao pamoja na wanadamu kuegemea kwa michezo ya ngono kunatoa ithibati kwamba waume na wanawake wanatafuta raha iliyo finyu katika ngono. Kitabu cha Warumi kinatoa msururu halisi wa namna wanadamu huangukia  uharibifu wanapoacha ile tabia halisi ya Mungu na kutafuta raha na kujitosheleza ambako ni kinyume na mpango halisi wa Mungu. Je, mpango wa Mungu ni upi kuhusu raha na uhusiano  wa ndoa? Je Bibilia inatoa maoni yapi kuhusu ngono ya jinsia moja? Je, mtu atafanyaje anapokumbwa na talaka na kuoa au kuolewa tena? Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo yameshughulikiwa katika kitabu hiki.