Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Des 09, 2020
Vya kupakuliwa 644

Lugha Zingine

български език Čeština English Français Deutsch Español

“Katika harakati zote kuu za kidini tangu siku za mitume, hakuna ambayo imekuwa huru kutoka kwa kasoro za wanadamu na hila za Shetani kuliko ilivyokuwa ile ya vuli ya 1844. Hata sasa, baada ya miaka mingi kupita, wote ambao walishiriki katika harakati hiyo na ambao wamesimama dhabiti juu ya jukwaa la kweli bado wanahisi athari takatifu ya kazi hiyo ambayo imebarikiwa na kushuhudia kwamba ilikuwa ya Mungu.” Great Controversy, ukurasa 402.

“Nilipokuwa nikiomba katika madhabahu ya familia, Roho Mtakatifu alikuja juu yangu, na nilionekana kuinuka juu zaidi, juu kuliko ulimwengu wa giza. Niligeuka kutafuta Waadventista ulimwenguni, lakini sikuwaona, ndipo sauti ikasema kwangu, "Angalia tena, na angalia juu kidogo." Katika hili niliyainua macho yangu, na nikaona njia iliyonyooka na nyembamba, ikiwekwa juu ya ulimwengu. Juu ya njia hii Waadventista walikuwa wakisafiri kwelekea kwenye mji, ambao ulikuwa mbali kwenye mwisho wa njia. Walikuwa na mwanga uliong’aa uliowekwa nyuma yao kwenye mwanzo wa njia, ambao malaika aliniambia ulikuwa kelele ya usiku wa manane. Nuru hii iliangaza njia yote na kutoa nuru kwa miguu yao ili kwamba wasijikwae. Kama wangeweka macho yao kwa Yesu, ambaye alikuwa mbele yao, akiwaongoza kuelekea kwa mji, wangekuwa salama.” Early Writings, Ukurasa 14.