Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jan 14, 2022
32
Vya kupakuliwa 275

Lugha Zingine

عربى English Français Deutsch Português Română

Na kwa hiyo ni jambo lisilochukulika kabisa kuwa Mungu yuko tayari leo kuteseka kwa ajili ya vifo vya watoto wachanga 125,000 ambao hawajazaliwa, 3000 waliokufa kwa kujiua, Elfu tatu na nusu waliouawa kwa ajali ya magari leo, maelfu na maelfu ambao wamekufa kwa kuzidiwa na madawa ya kulevya leo na maumivu na machungu yote ambayo yameambatana na mauaji hayo. Ameyavumilia yote hayo siku hii ya leo, ili kwamba uweze kupata siku nyingine ya kuishi na kumpa Kristo moyo wako na kujitoaa mwenyewe kikamilifu kwake ili kwamba Kristo, tumaini la utukufu apate kuumbika ndani yako.

Ili kwamba, Pale Kristo atakapodhihirishwa kikamilifu katika wale 144,000, kama ufunuo 14:1 isemavyo, wametiwa muhuri wa jina la Baba, ambalo ni tabia yake, ambayo imeandikwa katika amri 10, ndipo sasa tutakapoweza kwenda nyumbani. Lakini mpaka Injili hii ya Ufalme itakapohubiriwa. “Na injili hii ya ufalme itahubiriwa katika mataifa yote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote ndipo ule mwisho utakapokuja.” Ni injili ya kujikana nafsi. Ni injili ya kujikana nafsi kusikotamkika. Na kwa kumtazama Mungu wa injili hii, utaweza kubadilishwa na kufanana na sura yake, ikiwa utaiamini. Na unaweza kuanza kujikana nafsi na kuanza kuomba na kusali kwa ajili ya Roho wa Mungu, kwa namna ambayo hujawahi kuomba kabla, “Bwana, Nataka kufanana nawe.”