Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Des 13, 2019
imeandikwa Des 13, 2019
Vya kupakuliwa 1,115

Lugha Zingine

Afrikaans български език Čeština English Français Deutsch 國語 Српски Español

Mfumo wa kutoa sadaka na kafara yake ya wanyama na sadaka ya nyama na vinywaji vyote viliashiria neema ya uzima ya Yesu kupitia kwa huduma yake msalabani na upatanishi wake mbinguni kwa ajili yetu.

Swali linazuka ni nini umuhimu wa uzito na vipimo vya unga na mafuta na viwango vya wanyama? Kama matukio haya yote yaliashiria kifo cha Yesu miaka 2000 iliyopita basi ni jinsi gani kila ya hizi kafara za wanyama na nyama zilitofautiana kwa kila kusanyiko la kidini? Hili linamaana gani?

Kuna mafunzo kwetu katika kafara na sadaka hizi ambayo lazima tuzingatie?

Sheria ni injili ilivyo, na injili ni sheria iliyofunuliwa. Sheria ni mzizi, injili ni maua ya harufu nzuri na matunda ambayo huzaa. Agano la Kale hutoa nuru kuhusu Agano Jipya, na Jipya dhidi ya Kale. Kila moja ni ufunuo wa utukufu wa Mungu katika Kristo. Kila ukweli wa kisasa ambao utaendelea kudhihirisha ukweli mpya wa ndani kwa kwa mtafutaji asiyechoka. ukweli katika Kristo na kupitia kwa Kristo hauna kipimo. Wanafunzi wa maandiko hutafuta, jinsi ilivyo, katika chemchemi ambayo huongezeka kwa kina na upana anavyochungulia kina chake. Christ’s Object Lessons 128.

Tuweze kujifunza injili zaidi kupitia kwa nuru inayopatikana katika Agano la Kale. Wacha tunywe kutoka kwa chemchemi na tuzidishe kina cha furaha yetu katika injili ya Kristo.