Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Mac 09, 2020
imeandikwa Mac 09, 2020
Vya kupakuliwa 638

Maneno ambayo Baba alizungumza na Mwanawe wakati wa Ubatizo wake yanafanana na baraka aliyomimina juu ya Sabato ya kwanza ya Uumbaji. Kila siku Baba alifurahia Mwana wake, na Mwana alifurahia mbele Yake. Siku ya Sabato baba alimpulizia upendo wake Mwanawe na Mwana alirudishwa katika upendo wa Baba yake. Uhusiano huu wa karibu kati ya Baba na Mwana uliwekwa milele katika Sabato, na kila Sabato Baba humpulizia Mwana wake burudani ya pumziko na wale wote wanaomkubali Mwana wake.

Upendo wa Baba kwa Mwanawe ni wa kawaida, lakini unaonyeshwa kwa nyakati fulani zilizowekwa ambazo zinaonyesha kanuni ya Sabato. Tunapokuja kwa miadi hii tunaingia katika raha ya Baba kwa Mwana wake. Tunapo kuwa sehemu ya mwanamke anayesimama juu ya mwezi na amevikwa jua tunajua nyakati na majira ya kuburudisha yaliyotumwa kutoka kwa kiti cha enzi cha Baba yetu.

Baba yetu sasa anatuita katika uzoefu kamili wa Sabato. Tumeitwa katika baraka zote za kiroho katika Kristo Yesu kama watoto wa Abrahamu. Yesu anatuambia, “Tazama mimi nasimama mlangoni na ninapiga hodi” na Yeye anagonga wakati uliowekwa. Je! Utamfungulia Yeye na kula naye?