Wakarudia maksimu kuu mbili, kwamba sheria ni nakala ya ukamilifu wa kiungu, na kwamba mtu ambaye hampendi sheria haipendi injili; kwa kuwa sheria, na injili pia ni kioo kinachoonyesha tabia halisi ya Mungu. GC 465
Upendo na heshima na ukamilifu uliofunuliwa katika Injili ni ufunuo kwa mwanadamu wa tabia ya Mungu. Haki na wema na fadhili ambazo zilionekana katika tabia ya Kristo zinapaswa kurudiwa katika maisha ya wale wanaokubali haki za Injili. Kwa kusoma neno, tunapaswa kumuona jinsi alivyo, na, tukivutiwa na mtazamo wa ukamilifu wake wa Kiungu, tutakua katika sura ileile. Tunahitaji kuelewa kwamba Injili inadhihirisha kikamilifu utu [tabia] wa Bwana. Ni kioo kinachoonyesha tabia ya Mungu kwa roho iliyogeuzwa. Mfano wa Mungu umefunuliwa katika tabia kamilifu ya Mwana wake, ili tuweze kuelewa maana ya kufanywa kwa sura ya Mungu, na nini tunaweza kuwa ikiwa kwa kutazama daima tunajiruhusu kubadilishwa kutoka "utukufu kwa utukufu." ST Februari 24, 1909