Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Feb 26, 2020
imeandikwa Feb 26, 2020
Vya kupakuliwa 734

Je, kauli kama hizi twazichukuliaje?

Mbele za Mungu, malaika wote wana nguvu zaidi. Wakati mmoja kwa kumtii Kristo, waliangamiza wanajeshi wa Ashuri katika usiku mmoja, wanajeshi mia moja themanini na tano elfu. DA 702

Malaika Yule aliyetumwa kumwokoa Petero kifungoni kwa wakuu wa nchi, ndiye Yule aliyetekeleza ghadhabu iliyompata Herode. Malaka huyu alimgonga Petero ili kumwamsha, na kwa kichapo tofauti alimgoga Mfalme Herode, huku akipunguza kiburi chake na kukiweka chini, kichapo cha Mwenyezi Mungu. Basi Herode akafa kifo cha uchungu katika mawazo yake na mwili, kutokana na ghadhabu ya Mungu. " [AA 152]

Je, malaika watakatifu wa Mungu huua watu kweli? Je, Kristo kweli anayazungumza maneno haya? "Watu hawa lazima wafe sasa, nendeni mkawaue!" Je, Kristo alificha tabia hii ya Mungu alipokuja hapa duniani? Kristo hakuua yeyote alipokuwa hapa duniani. Kama kuua ni sehemu ya tabia yake, kwa nini haikujitokeza alipokuwa hapa duniani?

Luka 9:56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

Yohana 14:9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?