Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Sep 04, 2019
imeandikwa Sep 04, 2019
Vya kupakuliwa 1,080
Sauti za kupakuliwa 213
Jumla ya vilivyopakuliwa 1,293

Yeye aliye na Mwana anaouzima. Mbona hili liko hivyo? Kwa maana katika Mwana wa Mungu panaishi moyo mtakatifu wa Mwana mtiifu kwa Baba yake. Daima anafanya mambo ambayo yanampendeza Baba.  Pia anayomibaraka na upendo wa kina wa Baba. Moyo wa Mwana unapumzika kikamilifu katika upendo wa Baba yake.

Ni hekima ya Baba kugawa Roho wa Mwanawe mpendwa kwa ulimwengu; Roho tamu, wa upole na mtiifu ambaye anapenda amri za babake. Kristo ni hekima ya Mungu na usalama wa kupenda ufalme wa mahusiano.

Roho huyu mpole anatiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu kupitia kwa mti wa uzima. Shetani alimkataa Mwana wa Mungu na Roho wake wa upole. Roho wake wa uasi alikuwa vitani na Roho mpole, mnyenyekevu na mtiifu wa Mwana wa Mungu. Roho huyu wa uasi alipitishwa kwa jamii ya mwanadamu. Katika kafara ya Kristo tunapewa tena Roho huyu mpole. Siri ya kuwa na Roho huyu ni kujua Baba na Mwana ni akina nani – huu ni uzima wa milele kumjua Baba na Mwanawe na kunywa kutoka  kwa chemchemi ya maji ya uzima yanayobubujika kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwana kondoo.