Kudhihirisha Tabia ya Kutokuwa na Vurugu na ya Pumziko
Baba na Mwana Mzaliwa
Karibu kwenye Maranatha Media - Kenya.
Tuna furaha umefika hapa. Katika tovuti hii tunawapa vifaa vyetu bora kuhusu tabia ya Mungu wetu wa huruma na wa upendo - na unavyosoma, utafahamu kwa nini tuna uhakika kwamba Mungu kweli ni upendo. Kuna mengi ambayo watu hawafahamu kuhusu tabia ya Mungu - hata Wakristo thabiti! Shetani amefanya juu chini (na mara nyingi amefaulu) kuwafanya watu waamini kwamba Mungu ana tabia yake (Shetani) mwenyewe ambazo ni za hasira, kulipiza kisasi na mauaji badala ya tabia za Mungu mwenyewe ambazo tumeambiwa katika Biblia: upendo, mwingi wa rehema tena mwenye fadhili.
"Je, tuseme nini kuhusu hadithi za Biblia katika Agano la Kale kwamba Mungu anaua na kuamrisha mauaji?" Unaweza kuuliza. Nasi pia tumejiuliza suala hilo - kwa sababu Mungu kama huyo halingani na Yesu aliyefunuliwa katika Agano Jipya - tena hili ni wazo la kutatanisha kwa kila mtu anayetaka kuelewa kwa nini Mungu ni upendo.
Kile utakachogundua katika tovuti hii, ni matokeo ya utafiti wa miaka 16 kutaka kujua kuhusu Mungu na Yeye ni nani kwa uhakika. Kila kitabu kinadhihirisha uchunguzi wa Biblia kwa makini na kwa undani zaidi kuhusu mada husika. Ni tumaini letu kwamba vitakuwa baraka kwako kama vilivyo kwetu. Kuna uhuru na furaha kufahamu kwa uhakika ya kwamba Mungu wetu kweli ni Mungu wa upendo, na tunapendwa kwa undani na Yeye.