Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jul 07, 2020
Vya kupakuliwa 909

Lugha Zingine

Afrikaans български език Čeština English Français Deutsch 國語

Dada White katika maono mawili alionyeshwa jambo fulani kuhusiana na saa ya kuanza sabato. Maono ya kwanza yalikuwa mapema 1847, kule Topsham, Me. Katika maono hayo alionyeshwa kwamba kuanza sabato jua lichomozapo ni kosa. Kisha akasikia malaika akirudia maneno haya “Tangu jioni hata jioni mtasherehekea sabato zenu”.

Katika maono ya kwanza, tulielekezwa kawa neno la Mungu kwa maneno, “Tangu jioni hata jioni”, lakini kwa maoni ya wengi ikakubaliwa kwamba jioni ni saa kumi na mbili. Katika maono ya pili, maneno yale yale yalitumiwa na tulielekezwa haswa katika neno la Mungu, ambapo saa ya jioni ilichunguzwa zaidi. Hili lilimaliza suala hili tata na Kaka Bates na wengine na hili lilileta utulivu katika suala hili. James White, RH Feb, 25, 188

Itakuwa Sabato yenu ya kupumzika, nanyi mtaitesa mioyo yenu: siku ya tisa ya mwezi jioni, kutoka jioni hata jioni, mtaadhimisha Sabato yenu. Mambo ya Walawi 23:32

Lakini mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, kuweka jina lake, hapo utatoa dhabihu la pasaka jioni, jua likitua, wakati uliyokuwa ukitoka kutoka Misri. Kumb 16:6.