Maranatha Media Kenya
Iliyochapishwa Aug 29, 2021
20
Vya kupakuliwa 520

Wakristo wengi wana mawazo mengi kuhusu hasira na hukumu za Mungu, kuhusu matendo yake, kisasi chake na kichapo chake. Wao huamini kwamba wanamzungumzia Mungu ambaye hughadhabika wakati mwingine na kuwaadhibu kwa kuwaondoa wenye dhambi wakiukao sheria yake  kwa kuwaagiza malaika wake waue, wadhuru na kuwatesa wenye  dhambi. Je, watu hufikia kuamini haya vipi?

Kupitia hadithi za msalaba wa Kristo, na kuharibiwa kwa Yerusalemu, tunatambua muundo wa hukumu za Mungu na kule kuharibiwa kwa waovu mwishoni mwa dunia.

  1. Mungu huonya, kurekebisha na kuongoza kwa njia iliyo salama.
  2. Wanadamu hufuata njia zao, bila mwongozo wa Roho wa Mungu.
  3. Hata baada ya maonyo mengi, wanadamu bado hufuata njia zao.
  4. Wao hujiweka mbali na kinga za Mungu.
  5. Mungu huondoa Baraka zake na kinga zake.
  6. Roho wa Mungu huondolewa.
  7. Mungu hawaagizi malaika zake kuzuia mishale ya yule mwovu.
  8. Nguvu za shetani zinaafanya kazi baharini, ardhini, zikileta maangamizi na kilio zikimaliza umati mkubwa.