Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jan 13, 2023
Vya kupakuliwa 153

Lugha Zingine

English Deutsch

Kila mtu katika ulimwengu huu ana uhuru wa kuchagua kujitoa kwa Mungu na kushika amri zake kwa njia ya neema ya Kristo au kupinga na kukuza tabia ya uasi isiyofaa mbinguni.

Tuko katika saa za mwisho za historia ya dunia. Kila uamuzi tunaochukua kuanzia hatua hii kwenda mbele unatupeleka kwenye uzima wa milele au kifo cha milele. Apandavyo mtu ndivyo atakavyovuna. Mshahara wa dhambi ni mauti - mauti ya milele na zawadi ya Mungu ni uzima wa milele.

Hakuna nafasi baada ya maisha haya ya sasa kubadili tabia yako. Leo kama mtaisikia sauti yake msifanye migumu mioyo yenu bali mtafuteni Bwana maadamu anapatikana. Sasa tunapaswa kufanya wito wetu na uteule wetu kuwa wa uhakika kwa mara tu tunapokufa au Yesu akija hakutakuwa na nafasi tena ya kubadilika. Tabia zetu zitawekwa milele ama kwa kifo au kwa uzima.