Maranatha Media Kenya
Iliyochapishwa Sep 13, 2022
Vya kupakuliwa 50

Lugha Zingine

Čeština English Español

“Mimi ndimi ufufuo na uzima.” Katika ujuzi wetu juu ya Kristo na upendo wake ufalme wa Mungu umewekwa katikati yetu. Kristo anafunuliwa kwetu katika mahubiri na kuimbwa kwa nyimbo. Karamu ya kiroho imewekwa mbele yetu kwa wingi sana. Vazi la harusi, linalotolewa kwa gharama isiyo na kikomo, hutolewa bure kwa kila mtu. Kwa njia ya wajumbe wa Mungu tumeonyeshwa haki ya Kristo, kuhesabiwa haki kwa imani, ahadi kuu na za thamani za neno la Mungu, njia ya kumkaribia Baba kwa njia ya Kristo, faraja ya Roho Mtakatifu, uhakikisho wa uzima wa milele ulio na misingi imara katika ufalme wa Mungu. Mungu angeweza kutufanyia nini ambacho hajafanya katika kuandaa karamu kuu, karamu ya mbinguni? COL 317

Unaalikwa kwenye ufalme huu, mahali hapa pa thamani palipofunuliwa katika Kristo na palipo wazi kabisa kwa kila mwanamume, mwanamke na mtoto. Ufalme huu hauji kwa kuutazama kwa nje kwa kuwa ni ufalme wa kiroho unaonenwa kwa sauti ndogo tulivu. Kwa asili mwanadamu ni kiziwi, kipofu na anayepinga ufalme huu lakini katika uso wa Yesu Kristo umefunguliwa kwetu. Je, utakuja kwenye Karamu ya mbinguni?