Maranatha Media Kenya
Mwandishi W.W. Prescott
Iliyochapishwa Feb 16, 2024
Vya kupakuliwa 64

Lugha Zingine

English

Nini Kilifanya Kichaka na Mlima Kuwa Takatifu?

Musa alipokuwa kwenye kijiti kilichowaka moto, kama ilivyoandikwa katika sura ya tatu ya Kutoka, Bwana akamwambia, “Vua viatu vyako miguuni mwako, kwa maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu;” kwa Sababu Mwokozi - Muumba - alikuwepo. Basi Yoshua alipokutana na jemadari wa jeshi la Bwana, kama ilivyoandikwa katika sura ya tano ya Yoshua, alisema, “Vua viatu vyako miguuni mwako, kwa maana mahali hapo unaposimama ni patakatifu;” kwa sababu Kristo alikuwepo.

Bwana aliposhuka juu ya Mlima Sinai, mlima wote ulifanywa kuwa mtakatifu kwa uwepo wake maalum. Mlima huo haukuwa tofauti kabisa na sehemu nyingine zote za nchi kandokando, mpaka BWANA alipoufanya kuwa mtakatifu kwa uwepo wake. Alipokwisha kuzunguka kwa njia hiyo na kushuka juu yake, ndipo sehemu hiyo ya nchi ikawa takatifu, kwa sababu kuwapo kwake kulikuwa huko.