Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jun 06, 2021
28
Vya kupakuliwa 517

Lugha Zingine

عربى български език Čeština English Français Deutsch 國語 Српски Español

Naye Bwana akasema kwake, nenda kati ya mji na ukaweke alama kwenye vipaji vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. (5) Na hao wengine aliwaambia nami nilisikia, piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; (6) Waueni kabisa, mzee na kijana na msichana, na watoto wachanga, na wanawake, lakini msikaribie mtu yeyote aliye na alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Ezek 9:4­6

Je, Mungu anaagiza wanaume waue wasichana, watoto wadogo kwa kutumia vifaa vya kuua? Hili linafanana vipi na tabia ya Mungu aliyotoa Yesu?

Wana wa Iraeli walihusika sana katika ibada ya sanamu. Amri kumi zinatueleza namna Mungu anavyoshughulikia ibada ya sanamu.

Kutoka 20:5 Usivitumikie wala kuvisujudia; kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; ninawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao;

Je ina maana gani kuwaletea wana uovu wa baba zao na hili linahusiana vipi na Ezekieli tisa na mwisho wa dunia?