Maranatha Media Kenya
Mwandishi Gavin Devlin
Iliyochapishwa Apr 29, 2021
Vya kupakuliwa 506

Lugha Zingine

Afrikaans ဗမာ English bahasa Indonesia 國語 नेपाली Español

Kikao cha jioni kando ya moto wa kambi huhisika kuwa kizuri. Na kama mtu ambaye haupendi yuko pale? Saa hizo chache zitakuwa za wasiwasi kwa wahusika wote.

Sasa fikiria kukaribishwa kuishi milele katika moto wa kambi ya Mungu mbinguni. Lakini umesikia mambo mengi mabaya kumhusu... mbona utake kukaa milele na mtu mwenye kudhibiti na mwenye hasira, mtu ambaye haumpendi? Vizuri, hiyo ni hitimisho yako kumhusu Mungu kutokana na kile ambacho umesikia kutoka kwa Wakristo na wasio-Wakristo sawia. 

Na lakini kama sote tumedanganywa? Na kama sio mthibiti mkaidi jinsi watu wamemfanya kuwa? Na kama yeye ni Baba ambaye kwa kweli anawatakia wanawe mema tu, anataka kuwa karibu nao?  Anawezaje badilisha mtazamo wetu potovu na kuweka ndani yetu hamu yakuwa nyumbani na Baba? Tazama Baba yetu wa Mbinguni anapojaribu kuweka vitu sawa kwa ajili yetu, akitarajia tutabadilisha mawazo yetu kumhusu. Kamwe hajabadilisha mawazo yake kutuhusu.