Maranatha Media Kenya
Mwandishi Adrian Ebens
Iliyochapishwa Jan 17, 2023
32
Vya kupakuliwa 283

Lugha Zingine

български език Čeština English Deutsch 國語 Српски Español

Kristo alipomwomba Baba yake alitukuze jina lake, Baba alijibu kwamba amelitukuza na atalitukuza tena. Wakati Mungu alipozungumza, wengine walifikiri ilikuwa ni ngurumo na ilhali wengine walidhani ni malaika akizungumza na Kristo.

Tunapotafakari somo la mapigo ya Misri wengi husema kwamba ilinguruma, lakini katika mwanga wa injili kuna sauti tamu ya malaika inayotuhubiria msalaba wa Kristo. Injili ilihubiriwa kwa Israeli na sisi pia. Ebr 4:2

Kupitia kazi Yake ya upatanishi, Kristo alikuwa amewasihi kwa muda mrefu watu wa Misri. Alisimama katika pengo linalozidi kupanuka la ukengeufu hadi hatimaye mahitaji ya mharibifu yalibidi yatimizwe. Katika mauaji ya huzuni ya Misri tunasikia mwangwi wa nyayo za Mwokozi kuelekea msalabani. Katika kuinuliwa kwa fimbo ya nyoka tabia ya mharibifu ilifunuliwa kama vile pia upendo usio na ubinafsi wa Mungu na Mwanawe. Kweli, watu wote wanavutwa kwa Kristo katika nuru hii.

Tazama ng'ambo ya ngurumo, mvua ya mawe na damu na uone humu picha ya Mwana wa Mungu anayeteseka aliyejeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu na kuchubuliwa kwa ajili ya maovu yetu.