Ndani ya kila mmoja wetu ni hamu ya Amani, utulivu na dhibitisho la kupendwa. Ni jinsi gani jamii ya mwanadamu inaweza ukaribia uhalisia huu? Na maendeleo haya yote katika teknolojia ulimwengu wetu yanaingia ndani zaidi katika ubinafsi na ukatili.
Maisha ya Kristo ambaye alitembea duniani miaka 2000 iliyopita yanatupa mfano wa upendo wa kujikana nafsi ambao umeleta amani kwa mamilioni yasiyohesabika. Kwa watu wengi upendo huu mzuri huangamizwa na hata kuharibiwa na hadithi nyingi ambazo zimenakiliwa katika kurasa za Bibilia zikielezea uhusiano wa Mungu na watu katika historia yote ya mwanadamu.
Mungu wakati mwengine huonekana kuwa mkatili kabisa na muuaji aamuruye sio tu kifo cha majeshi ya adui bali pia watoto wao wachanga. Huonyesha kwa utaratibu wa kuogofya kuwa amekasirika na kujawa na ghadhabu. Zaidi ya hili kifo cha msalaba ni kwa wengi kuchafuliwa na mawazo kuwa Mungu huhitaji kifo kwa wale wanaomuasi.
Kwa walio na mvuto kwa neno la Mungu, tofauti kati ya maelezo ya Mungu na maisha ya Kristo imesababisha baadhi ya madai ya Yesu kuwa gumu Zaidi kutatua. Ila katika kipindi fulani akinena kwa mmoja wa wafuasi wake Yesu alisema, “Iwapo umeniona umemwona Baba.”
Hili linawezekanaje? Inaweza kuwa ukweli kuwa Mungu kwa kweli ni mwenye huruma, neema na ukarimu kama inavyodhihirishwa katika maisha ya Yesu? utata huu unaweza tatuliwa katika kusalia waaminifu kwa neno la Andiko? Unashikilia mikononi mwako ufunguo wa kufungua after hii.