
Swala kuhusu sheria kuwa sheria kwa Wagalatia ilikuwa ni kiini cha vita vya mafundisho ambayo yaliyo kuwemo mwaka wa 1888 katika kongamano la Bibilia la Waadventista wa Sabato.
Je ni kwa nini ni muhimu kuelewa vidokezo vya kati kuhusiana na swala hili? Sheria katika Wagalatia inadhihirisha kama tunaelewa agano la milele vyema kulingana na undani wa maandiko. Ijapokuwa inawezekana kushika mada ya kati ya agano la milele, mada hii lazima ieleweke kwa undani wa maandiko ili kwa kweli ithaminiwe na kufundishwa kwa maandiko. Hii ni kweli hasa kulingana na maandishi ya Paulo.